KUHUSU KITUO CHA DAARUL HADITH UNUNIO
FAHAMU KUHUSU KITUO CHA DHUIC
UTANGULIZI
Darul Hadith Ununio Islamic Center (DHUIC) ni Taasisi ya Kidini iliyopata usajili 24/Oktoba/ 2017 ikiwa na Namba ya usajili 5348 kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) usajili huu unahusu wadhamini kwa ajili ya kusimamia mali mbalimbali za Taasisi. Aidha kwa sasa Taasisi ipo katika hatua ya kuomba usajili Wizara ya Mambo ya Ndani kufuatia maelekezo ya Serikali.
HISTORIA KWA UFUPI
Eneo hili lenye ukubwa wa takriban ekari tatu (3) lilitolewa Wakfu na Marehemu Mzee Khamisi Kambi kwa ajili ya shughuli za kidini.
Mnamo Mwaka 2000 eneo hili lilivamiwa na Wakristo wa madhehebu ya Assembles of God Tanzania (TAG) na kujenga Kanisa pamoja na nyumba ya mchungaji. Wakristo walienedsha ibada zao katika eneo hili kwa takriban miaka miwili.
Jamii ya Waislamu wanaoishi karibu na eneo hili walikua wakihangaika kutafuta eneo la kufanya ibada kwa kuwa Msikiti wa karibu na eneo hili upo takriban mita 800 au kilometa moja.
wakati wanatafuta eneo la karibu la kusali ndipo zikapatika taarifa kwamba eneo lililojengwa kanisa ni eneo la Waislamu lillilotolewa wakfu na kuvamiwa na wasio waislamu.
Baada ya hapo Waislamu wanaoishi maeneo haya walianzisha juhudi za kulikomboa eneo hilo kwa kushirikiana na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (Baraza Kuu) pamoja na Shura ya Maimam Tanzania.
Hatimaye Ardhi hiyo ya Wakfu ilikombolewa na kurejeshwa mikononi mwa waislamu. Baada ya Wakfu huo kurejeshwa hatua zilizofuatia kwanza ilikua kusajili Taasisi ndipo mnamo 24/Oct/2016 DHUIC ikapata usajili kupitia RITA. Hatua ya pili ilikuwa kufuatilia Hati miliki ya Wakfu huo Wizara ya Ardhi. Tarehe….hati miliki ilitolewa na Serikali kupitia Wizara husika. Hati ilitoka kwa jina la Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kwa niaba ya waumini wa Ununio kwa sababu kubwa mbili:
Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi haziruhusu Taasisi yoyote kufanya shughuli zake bila kupata usajili pamoja na kumiliki mali.
Mkutano wa Viongozi wa Ununio Islamic Center na Baraza Kuu uliazimia kwamba Hati ya Wakfu huu iandikishwe kwa jina la Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (Baraza Kuu) hadi hapo waumini wa Ununio Islamic Center watakapo kuwa wamesajili Taasisi yao. Baada ya hapo hati miliki itahamishwa toka Baraza Kuu na kwenda Ununio Islamic Center.